Skip to content
Mathayo 25:1-17

Mathayo 25:1-17

1
“Wakati huo, Ufalme wa Mbinguni utakuwa kama wanawali kumi waliochukua taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi.
2
Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara.
3
Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba,
4
lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo.
5
Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.
6
“Usiku wa manane pakawa na kelele: ‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!’
7
“Ndipo wale wanawali wote wakaamka na kuzitengeneza taa zao.
8
Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta yenu kidogo; taa zetu zinazimika.’
9
“Lakini wale wenye busara wakawajibu, ‘Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu.’
10
“Nao walipokuwa wakienda kununua mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa.
11
“Baadaye wale wanawali wengine nao wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’
12
“Lakini yeye bwana arusi akawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’
13
“Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa.
14
“Tena, Ufalme wa Mbinguni ni kama mtu aliyetaka kusafiri, naye akawaita watumishi wake na kuweka mali yake kwenye uangalizi wao.
15
Mmoja akampa talantatano, mwingine talanta mbili, na mwingine talanta moja. Kila mmoja alipewa kwa kadiri ya uwezo wake. Kisha yeye akasafiri.
16
Yule aliyepewa talanta tano akaenda mara moja akafanya nazo biashara akapata talanta nyingine tano zaidi.
17
Yule aliyepewa talanta mbili akafanya vivyo hivyo, akapata nyingine mbili zaidi.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options