Skip to content
Mathayo 22:34-40

Mathayo 22:34-40

34
Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, Mafarisayo wakakusanyika pamoja.
35
Mmoja wao, mtaalamu wa sheria, akamuuliza swali ili kumjaribu, akisema,
36
“Mwalimu, ni amri ipi katika Sheria iliyo kuu kuliko zote?”
37
Yesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’
38
Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
39
Nayo ya pili ni kama hiyo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’
40
Amri hizi mbili ndizo msingi wa Sheria na Manabii.”
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options