Skip to content
Mathayo 10:28-39

Mathayo 10:28-39

28
Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanamu.
29
Je, shomoro wawili hawauzwi kwa senti moja tu? Lakini hakuna hata mmoja wao atakayeanguka chini pasipo Baba yenu kujua.
30
Hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa.
31
Hivyo msiogope; kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.
32
“Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi nami nitamkiri yeye mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
33
Lakini yeyote atakayenikana mimi mbele ya watu, mimi nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.”
34
“Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.
35
Kwa maana nimekuja kumfitini “ ‘mtu na babaye, binti na mamaye, mkwe na mama mkwe wake;
36
nao adui za mtu watakuwa ni wale watu wa nyumbani kwake.’
37
“Yeyote ampendaye baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Yeyote ampendaye mwanawe au binti yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu.
38
Tena yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa wangu.
39
Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options