Luka 20:41-47
41
Kisha Yesu akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Kristoni Mwana wa Daudi?
42
Daudi mwenyewe anasema katika Kitabu cha Zaburi: “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume,
43
hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” ’
44
Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?”
45
Wakati watu wote walikuwa wanamsikiliza, Yesu akawaambia wanafunzi wake,
46
“Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kukaa kwenye nafasi za heshima katika karamu.
47
Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema, wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”
Settings