Waamuzi 5:1-11
1
Ndipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu:
2
“Wakuu katika Israeli wanapoongoza, wakati watu wanapojitoa kwa hiari yao wenyewe: mhimidini Bwana!
3
“Sikieni hili, enyi wafalme! Sikilizeni, enyi watawala! Nitamwimbia Bwana, nitaimba; kwa wimbo nitamhimidi Bwana, Mungu wa Israeli.
4
“Ee Bwana, ulipotoka katika Seiri, ulipopita katika mashamba ya Edomu, nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga, naam, mawingu yakamwaga maji.
5
Milima ilitetemeka mbele za Bwana, hata ule wa Sinai, mbele za Bwana, Mungu wa Israeli.
6
“Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi, katika siku za Yaeli, barabara kuu hazikuwa na watu; wasafiri walipita njia za kando.
7
Mashujaa walikoma katika Israeli, walikoma mpaka mimi, Debora, nilipoinuka, nilipoinuka kama mama katika Israeli.
8
Walipochagua miungu migeni, vita vilikuja katika malango ya mji, hapakuonekana ngao wala mkuki miongoni mwa mashujaa 40,000 katika Israeli.
9
Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli, pamoja na wale wanaojitoa wenyewe kwa hiari yao miongoni mwa watu. Mhimidini Bwana!
10
“Nanyi mpandao punda weupe, mkiketi juu ya matandiko ya thamani, nanyi mtembeao barabarani, fikirini
11
juu ya sauti za waimbaji mahali pa kunyweshea maji. Wanasimulia matendo ya haki ya Bwana, matendo ya haki ya mashujaa wake katika Israeli. “Ndipo watu wa Bwana walipoteremka malangoni pa mji.
Maandiko ya Biblia: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)™, © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. · CC BY-SA 4.0“Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc., used with permission.
Settings