Skip to content
Ayubu 40:10-19

Ayubu 40:10-19

10
Basi jivike mwenyewe utukufu na fahari, nawe uvae heshima na enzi.
11
Fungulia ukali wa ghadhabu yako, mtafute kila mwenye kiburi umshushe,
12
mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze, waponde waovu mahali wasimamapo.
13
Wazike wote mavumbini pamoja; wafunge nyuso zao kaburini.
14
Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa.
15
“Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi, niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe, anayekula majani kama ngʼombe.
16
Tazama basi nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake, uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake!
17
Mkia wake hutikisika kama mwerezi; mishipa ya mapaja yake imesukwa pamoja.
18
Mifupa yake ni bomba za shaba, maungo yake ni kama fito za chuma.
19
Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu, lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options