Ayubu 37:1-11
1
“Kwa hili moyo wangu unatetemeka, nao unaruka kutoka mahali pake.
2
Sikiliza! Sikiliza ngurumo ya sauti yake, sauti ya ngurumo itokayo kinywani mwake.
3
Huuachilia umeme wake wa radi chini ya mbingu yote na kuupeleka hata miisho ya dunia.
4
Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake; Mungu hunguruma kwa sauti yake ya fahari. Wakati sauti yake ingurumapo tena, huuachilia umeme wake wa radi.
5
Sauti ya Mungu hunguruma kwa namna za ajabu; yeye hutenda mambo makuu kupita ufahamu wetu.
6
Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’ nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’
7
Ili wanadamu wote aliowaumba wapate kujua kazi zake, yeye humzuilia kila mtu shughuli zake.
8
Wanyama hujificha; hubakia kwenye mapango yao.
9
Dhoruba hutoka katika chumba chake, baridi hutoka katika upepo uendao kasi.
10
Pumzi ya Mungu hutoa barafu, eneo kubwa la maji huganda.
11
Huyasheheneza mawingu kwa maji, naye husambaza umeme wake wa radi kupitia hayo.
Settings