Skip to content
Ayubu 18:5-17

Ayubu 18:5-17

5
“Taa ya mwovu imezimwa, nao mwali wa moto wake umezimika.
6
Mwanga hemani mwake umekuwa giza; taa iliyo karibu naye imezimika.
7
Nguvu za hatua zake zimedhoofishwa; shauri lake baya litamwangusha.
8
Miguu yake imemsukumia kwenye wavu, naye anatangatanga kwenye matundu ya wavu.
9
Tanzi litamkamata kwenye kisigino; mtego utamshikilia kwa nguvu.
10
Kitanzi kimefichwa ardhini kwa ajili yake; mtego uko kwenye njia yake.
11
Vitisho vimemtia hofu kila upande, na adui zake humwandama kila hatua.
12
Janga linamwonea shauku; maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo.
13
Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake; mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake.
14
Atangʼolewa kutoka usalama wa hema lake, na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.
15
Moto utakaa katika hema lake; moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake.
16
Mizizi yake chini itakauka na matawi yake juu yatanyauka.
17
Kumbukumbu lake litatoweka katika dunia, wala hatakuwa na jina katika nchi.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options