Skip to content
Yeremia 9:13-21

Yeremia 9:13-21

13
Bwana akasema, “Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu, niliyoiweka mbele yao: hawajaniheshimu mimi wala kufuata sheria yangu.
14
Badala yake wamefuata ukaidi wa mioyo yao, wamefuata Mabaali, kama vile baba zao walivyowafundisha.”
15
Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: “Tazama, nitawafanya watu hawa wale chakula kichungu na kunywa maji yenye sumu.
16
Nitawatawanya katika mataifa ambayo wao wala baba zao hawakuwajua, nikiwafuata kwa upanga mpaka niwe nimewaangamiza kabisa.”
17
Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Fikiri sasa! Waite wanawake waombolezao waje, waite wale walio na ustadi kuliko wote.
18
Nao waje upesi na kutuombolezea, mpaka macho yetu yafurike machozi na vijito vya maji vitoke kwenye kope zetu.
19
Sauti ya kuomboleza imesikika kutoka Sayuni: ‘Tazama jinsi tulivyoangamizwa! Tazama jinsi aibu yetu ilivyo kubwa! Ni lazima tuihame nchi yetu kwa sababu nyumba zetu zimekuwa magofu.’ ”
20
Basi, enyi wanawake, sikieni neno la Bwana; fungueni masikio yenu msikie maneno ya kinywa chake. Wafundisheni binti zenu kuomboleza; fundishaneni kila mmoja na mwenzake maombolezo.
21
Mauti imeingia ndani kupitia madirishani, imeingia kwenye majumba yetu ya fahari; imewakatilia mbali watoto katika barabara na vijana waume kutoka viwanja vya miji.

Maandiko ya Biblia: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)™, © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. · CC BY-SA 4.0“Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc., used with permission.

Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options