Isaya 23:1-7
1
Neno kuhusu Tiro: Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi! Kwa kuwa Tiro imeangamizwa, imeachwa bila nyumba wala bandari. Kuanzia nchi ya Kitimu neno limewajia.
2
Nyamazeni kimya, enyi watu wa kisiwani, pia ninyi wafanyabiashara wa Sidoni, ambao mabaharia wamewatajirisha.
3
Kwenye maji makuu nafaka za Shihori zilikuja; mavuno ya Naili yalikuwa mapato ya Tiro, naye akawa soko la mataifa.
4
Uaibishwe ee Sidoni, nawe ee ngome la bahari, kwa kuwa bahari imesema: “Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa wala sijapata kuzaa, wala sijapata kulea wana wala kutunza mabinti.”
5
Habari ifikapo Misri, watakuwa katika maumivu makuu kwa ajili ya taarifa kutoka Tiro.
6
Vukeni mpaka Tarshishi, ombolezeni, enyi watu wa kisiwani.
7
Je, huu ndio mji wenu uliojaa sherehe, mji wa zamani, zamani kabisa ambao miguu yake imeuchukua kufanya makao nchi za mbali sana?
Settings