Isaya 23:8-14
8
Ni nani amepanga hili dhidi ya Tiro, mji utoao mataji, ambao wafanyabiashara wake ni wana wa mfalme na wachuuzi wake ni watu mashuhuri wa dunia?
9
Bwana Mwenye Nguvu Zote ndiye alipanga jambo hili, ili kukishusha kiburi cha utukufu wote na kuwanyenyekesha wale wote ambao ni mashuhuri duniani.
10
Ee Binti Tarshishi, pita katika nchi yako kama vile Mto Naili kwa kuwa huna tena bandari.
11
Bwana amenyoosha mkono wake juu ya bahari na kuzifanya falme zake zitetemeke. Ametoa amri kuhusu Kanaani kwamba ngome zake ziangamizwe.
12
Alisema, “Usizidi kufurahi, ee Bikira Binti Sidoni, sasa umepondwa! “Simama, vuka uende Kitimu; hata huko hutapata pumziko.”
13
Tazama katika nchi ya Wakaldayo, watu hawa ambao sasa hawaonekani kama wapo! Waashuru wameifanya nchi hiyo kuwa mahali pa viumbe wa jangwani. Wamesimamisha minara yao ya vita kuuzunguka, wameziteka ngome zake na kuziacha tupu na kuufanya kuwa magofu.
14
Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi; ngome yenu imeangamizwa!
Settings