Mwanzo 10:8-12
8
Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani.
9
Alikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.”
10
Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari.
11
Kutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala,
12
na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.
Settings