Kutoka 39:32-42
32
Kwa hiyo kazi yote ya maskani, Hema la Kukutania ikakamilika. Waisraeli wakafanya kila kitu sawasawa kama vile Bwana alivyomwagiza Mose.
33
Ndipo wakaleta maskani kwa Mose: hema pamoja na vifaa vyake vyote, vibanio vyake, mihimili yake, mataruma yake, nguzo na vitako vyake;
34
kifuniko cha ngozi za kondoo dume kilichotiwa rangi nyekundu, kifuniko cha ngozi za pomboo, pazia la kufunikia;
35
Sanduku la Ushuhuda pamoja na mipiko yake na kiti cha rehema,
36
meza pamoja na vyombo vyake vyote na mikate ya Wonyesho;
37
kinara cha taa cha dhahabu safi, safu zake za taa pamoja na vifaa vyake vyote pamoja na mafuta kwa ajili ya taa;
38
madhabahu ya dhahabu, mafuta ya upako, uvumba wenye harufu nzuri na pazia la ingilio la hema;
39
madhabahu ya shaba, pamoja na wavu wa shaba, nguzo zake na vyombo vyake vyote, sinia, na tako lake;
40
mapazia ya ua pamoja na nguzo na vitako vyake, pia na pazia kwa ajili ya ingilio la kwenye ua; kamba zake na vigingi vya hema kwa ajili ya ua; vyombo vyote vilivyohitajiwa kwa ajili ya maskani, Hema la Kukutania;
41
na mavazi yaliyofumwa yanayovaliwa wakati wa huduma katika mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu ya kuhani Aroni na mavazi kwa ajili ya wanawe watakapokuwa wakihudumu katika kazi ya ukuhani.
42
Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile Bwana alivyokuwa amemwagiza Mose.
Settings