2 Wakorintho 10:1-9
1
Basi, mimi Paulo ninawasihi kwa unyenyekevu na upole wa Kristo, mimi niliye “mwoga” ninapokuwa pamoja nanyi ana kwa ana, lakini mwenye ujasiri nikiwa mbali nanyi!
2
Nawaomba nitakapokuja kwenu nisiwe na ujasiri dhidi ya watu fulani, kama ninavyotazamia kwa wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa kufuata namna ya ulimwengu huu.
3
Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo.
4
Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome,
5
tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo,
6
tena tukiwa tayari kuadhibu kila tendo la kutotii, kutii kwenu kutakapokamilika.
7
Angalieni yale yaliyo machoni penu. Kama mtu yeyote anaamini kuwa yeye ni mali ya Kristo, basi kumbuka kuwa kama ulivyo wa Kristo, vivyo hivyo na sisi ndivyo tulivyo.
8
Basi hata kama nikijisifu zaidi kidogo kuhusu mamlaka tuliyo nayo, ambayo Bwana alitupa ili kuwajenga wala si kuwabomoa, mimi sitaionea haya.
9
Sitaki nionekane kama ninayejaribu kuwatisha kwa nyaraka zangu.
Settings