Skip to content
1 Wafalme 13:14-19

1 Wafalme 13:14-19

14
na kumfuatilia yule mtu wa Mungu. Akamkuta ameketi chini ya mwaloni na akamuuliza, “Je, wewe ndiwe mtu wa Mungu kutoka Yuda?” Akamjibu, “Mimi ndiye.”
15
Basi nabii akamwambia, “Karibu nyumbani pamoja na mimi ule.”
16
Yule mtu wa Mungu akasema, “Siwezi kurudi na kwenda nawe, wala siwezi kula mkate au kunywa maji pamoja nawe mahali hapa.
17
Nimeambiwa kwa neno la Bwana: ‘Kamwe usile mkate au kunywa maji huko au kurudia njia uliyojia.’ ”
18
Yule nabii mzee akajibu, “Mimi pia ni nabii, kama wewe. Naye malaika alisema nami kwa neno la Bwana: ‘Mrudishe aje katika nyumba yako ili apate kula mkate na kunywa maji.’ ” (Lakini alikuwa akimwambia uongo.)
19
Hivyo mtu wa Mungu akarudi pamoja naye na akala na kunywa katika nyumba yake.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options