1 Nyakati 7:30-40
30
Wana wa Asheri walikuwa: Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera.
31
Wana wa Beria walikuwa: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.
32
Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao.
33
Wana wa Yafleti walikuwa: Pasaki, Bimhali na Ashvathi. Hawa walikuwa wana wa Yafleti.
34
Wana wa Shemeri walikuwa: Ahi, Roga, Yehuba na Aramu.
35
Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa: Sofa, Imna, Sheleshi na Amali.
36
Wana wa Sofa walikuwa: Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra,
37
Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani na Beera.
38
Wana wa Yetheri walikuwa: Yefune, Pispa na Ara.
39
Wana wa Ula walikuwa: Ara, Hanieli na Risia.
40
Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa walio hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa tayari kwa vita, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa 26,000.
Settings