Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu The Ostrich

9 mistari · 9 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. “ ‘Wafuatao ndio ndege watakaokuwa machukizo kwenu, hivyo msiwale kwa sababu ni chukizo: tai, furukombe, kipungu,

  2. Nimekuwa ndugu wa mbweha, rafiki wa mabundi.

  3. “Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa furaha, lakini hayawezi kulinganishwa na mabawa na manyoya ya korongo.

  4. Huyataga mayai yake juu ya ardhi, na kuyaacha yapate joto mchangani,

  5. bila kujali kuwa mguu waweza kuyaponda, kwamba baadhi ya wanyama wa porini wanaweza kuyakanyaga.

  6. Yeye huyafanyia makinda yake ukatili kama vile si yake; hajali kwamba taabu yake inaweza ikawa bure,

  7. kwa kuwa Mungu hakumjalia hekima, wala hakumpa fungu la akili njema.

  8. Lakini akunjuapo mabawa yake kukimbia, humcheka farasi pamoja na yeye aliyempanda.

  9. Hata mbweha hutoa matiti yao kunyonyesha watoto wao, lakini watu wangu wamekuwa wasio na huruma kama mbuni jangwani.