Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Feast of Pentecost

8 mistari · 14 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Mlete sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na pia wana-kondoo saba wenye umri wa mwaka mmoja, kama harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

  2. Pamoja na kila fahali itatolewa sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini;

  3. na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba.

  4. Ongeza beberu mmoja kwa kufanya upatanisho kwa ajili yenu.

  5. Andaa hizi sadaka pamoja na sadaka zake za vinywaji, kuwa nyongeza ya sadaka za kawaida za kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka. Hakikisha kuwa wanyama hao hawana dosari.

  6. Siku ya Pentekoste ilipowadia, waamini wote walikuwa mahali pamoja.

  7. Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali uliotoka mbinguni ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi.

  8. Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao.