Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Fall of Man: Through temptation of the devil

5 mistari · 34 vipengele

Mistari kuhusu Through temptation of the devil

  1. Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao Bwana Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?”

  2. Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini,

  3. lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ ”

  4. Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa.

  5. Kwa maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”