Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Miriam: Watches over Moses when he is in the ark

5 mistari · 4 vipengele

Mistari kuhusu Watches over Moses when he is in the ark

  1. Dada ya huyo mtoto akasimama mbali ili kuona kitakachompata mtoto.

  2. Ndipo binti Farao akateremka mtoni Naili kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti mfalme akaona kisafina katikati ya manyasi, akamtuma mmoja wa watumwa wake wa kike kukichukua.

  3. Alifungua kisafina akaona mtoto ndani yake. Mtoto alikuwa akilia, akamhurumia. Akasema, “Huyu ni mmoja wa watoto wa Kiebrania.”

  4. Ndipo dada wa huyo mtoto akamuuliza binti Farao, “Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Kiebrania akulelee huyu mtoto?”

  5. Binti Farao akamjibu, “Ndiyo, nenda.” Yule msichana akaenda akamleta mama wa mtoto.