Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Jephthah: Leads the host of Israel against the Ammonites

5 mistari · 12 vipengele

Mistari kuhusu Leads the host of Israel against the Ammonites

  1. Ndipo Roho wa Bwana akaja juu ya Yefta. Akapita katikati ya Gileadi na Manase, pia akapita katika Mispa ya Gileadi, na kutokea huko akasonga mbele kushambulia Waamoni.

  2. Naye Yefta akaweka nadhiri mbele za Bwana akisema, “Ikiwa utawatia Waamoni mikononi mwangu,

  3. chochote kile kitakachotoka katika mlango wa nyumba yangu cha kwanza ili kunilaki nirudipo kwa amani katika kuwashinda Waamoni, kitakuwa ni cha Bwana na nitakitoa kuwa sadaka ya kuteketezwa.”

  4. Ndipo Yefta akavuka kupigana na hao Waamoni, naye Bwana akawatia mkononi mwake.

  5. Akawapiga kwa ushindi mkubwa kuanzia Aroeri mpaka karibu na Minithi na kuendelea mpaka Abel-Keramimu, miji yote iliyopigwa ni ishirini. Basi Israeli wakawashinda Waamoni.