Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Happiness of Saints In This Life: Described by Christ in the beatitudes

10 mistari · 19 vipengele

Mistari kuhusu Described by Christ in the beatitudes

  1. “Heri walio maskini wa roho, maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.

  2. Heri wale wanaohuzunika, maana hao watafarijiwa.

  3. Heri walio wapole, maana hao watairithi nchi.

  4. Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watatoshelezwa.

  5. Heri wenye huruma, maana hao watapata rehema.

  6. Heri walio na moyo safi, maana hao watamwona Mungu.

  7. Heri walio wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.

  8. Heri wanaoteswa kwa sababu ya haki, maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.

  9. “Heri ninyi watu watakapowashutumu, na kuwatesa na kunena dhidi yenu mabaya ya aina zote kwa uongo kwa ajili yangu.

  10. Furahini na kushangilia kwa maana thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.