Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Conscience: The blood of Christ alone can purify

9 mistari · 15 vipengele

Mistari kuhusu The blood of Christ alone can purify

  1. Kama dhabihu hizo zingeweza kuwakamilisha, hazingeendelea kutolewa tena. Kwa kuwa hao waabuduo wangekuwa wametakaswa mara moja tu, wala wasingejiona tena kuwa na dhambi.

  2. Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka,

  3. kwa sababu haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

  4. Kwa hiyo, Kristo alipokuja duniani, alisema: “Dhabihu na sadaka hukuzitaka, bali mwili uliniandalia;

  5. sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukupendezwa nazo.

  6. Ndipo niliposema, ‘Mimi hapa, nimekuja, imeandikwa kunihusu katika kitabu: Nimekuja kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu.’ ”

  7. Kwanza alisema, “Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo” (ingawa sheria iliagiza zitolewe).

  8. Kisha akasema “Mimi hapa, nimekuja kuyafanya mapenzi yako.” Aondoa lile Agano la kwanza ili kuimarisha la pili.

  9. Katika mapenzi hayo sisi tumetakaswa na kufanywa watakatifu kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu.