Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Bridegroom: Song of

10 mistari · 7 vipengele

Mistari kuhusu Song of

  1. Wewe ni mzuri kote, mpenzi wangu, hakuna hitilafu ndani yako.

  2. Enda nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu, enda nami kutoka Lebanoni. Shuka kutoka ncha ya Amana, kutoka juu ya Seniri, kilele cha Hermoni, kutoka mapango ya simba na kutoka mlima wapendapo kukaa chui.

  3. Umeiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu; umeiba moyo wangu kwa mtazamo mmoja wa macho yako, kwa kito kimoja cha mkufu wako.

  4. Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha, dada yangu, bibi arusi wangu! Pendo lako linafurahisha aje zaidi ya divai, na harufu ya manukato yako zaidi ya kikolezo chochote!

  5. Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali, bibi arusi wangu; maziwa na asali viko chini ya ulimi wako. Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni.

  6. Wewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu, bibi arusi wangu; wewe ni chanzo cha maji kilichozungushiwa kabisa, chemchemi yangu peke yangu.

  7. Mimea yako ni bustani ya mikomamanga yenye matunda mazuri sana, yenye hina na nardo,

  8. nardo na zafarani, mchai na mdalasini, pamoja na kila aina ya mti wa uvumba, manemane na udi, na aina zote za vikolezo bora kuliko vyote.

  9. Wewe ni chemchemi ya bustani, kisima cha maji yatiririkayo, yakitiririka kutoka Lebanoni.

  10. Amka, upepo wa kaskazini, na uje, upepo wa kusini! Vuma juu ya bustani yangu, ili harufu yake nzuri iweze kuenea mpaka ngʼambo. Mpendwa wangu na aje bustanini mwake na kuonja matunda mazuri sana.