Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Blasphemy: General references

81 mistari · 19 vipengele

Mistari kuhusu General references

Chuja kwa kitabu
  1. Basi mwana wa mama Mwisraeli na baba Mmisri alikwenda miongoni mwa Waisraeli, nayo mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli.

  2. Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru Jina la Bwana kwa kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Mose. (Jina la mama yake aliitwa Shelomithi binti wa Dibri, wa kabila la Dani.)

  3. Nao wakamweka mahabusu mpaka mapenzi ya Bwana yawe wazi kwao.

  4. Ndipo Bwana akamwambia Mose:

  5. “Mchukue huyo aliyekufuru nje ya kambi. Wale wote waliomsikia akikufuru wataweka mikono juu ya kichwa chake, kisha kusanyiko lote litampiga mawe.

  6. Waambie Waisraeli: ‘Ikiwa mtu yeyote atamlaani Mungu wake, atakuwa na hatia kwa uovu wake;

  7. yeyote atakayekufuru Jina la Bwana ni lazima auawe. Kusanyiko lote litampiga kwa mawe. Iwe ni mgeni au mzawa, atakapolikufuru Jina la Bwana, ni lazima auawe.

  8. Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali, siamini kama angenisikiliza.

  9. Yeye angeniangamiza kwa dhoruba na kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu.

  10. Asingeniacha nipumue bali angenifunika kabisa na huzuni kuu.

  11. mtu angeliiondoa fimbo ya Mungu juu yangu, ili utisho wake usiendelee kunitia hofu.

  12. Ndipo ningenena naye, bila kumwogopa, lakini kama ilivyo kwangu sasa, sitaweza.

  13. Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu.

  14. Je, inakupendeza wewe kunionea, kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu?

  15. Je, wewe una macho ya kimwili? Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo?

  16. Je, siku zako ni kama zile za mwanadamu, au miaka yako ni kama ile ya mtu,

  17. ili kwamba utafute makosa yangu na kuichunguza dhambi yangu;

  18. ingawa wajua kuwa mimi sina hatia, na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako?

  19. Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu? Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake?

  20. Mtamwonyesha upendeleo? Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake?

  21. Je, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi? Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu?

  22. Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo? Je, utayasaka makapi makavu?

  23. Kwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu.

  24. Umeifunga miguu yangu kwenye pingu. Unazichunga kwa makini njia zangu zote kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu.

  25. kwa sababu amemkunjia Mungu ngumi yake na kujigamba dhidi ya Mwenyezi,