Rukia maudhui

Ahaziah

7 mistari · 5 wanafamilia

Mistari inayomtaja Ahaziah

  1. Ahabu akalala pamoja na baba zake. Naye Ahazia mwanawe akawa mfalme baada yake.

  2. Wakati ule, Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yehoshafati, “Waache watu wangu wasafiri baharini pamoja na watu wako,” lakini Yehoshafati akakataa.

  3. Ahazia mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye alitawala katika Israeli kwa miaka miwili.

  4. Basi Ahazia alikuwa ameanguka huko Samaria kutoka baraza ya chumba chake cha juu, akaumia. Hivyo akatuma wajumbe, akiwaambia, “Nendeni mkaulize kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni, mkaone kama nitapona kutokana na kuumia huku.”

  5. Kwa matukio mengine ya utawala wa Ahazia na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?

  6. Hatimaye Yehoshafati mfalme wa Yuda akafanya urafiki na Ahazia mfalme wa Israeli ambaye alifanya maovu sana.

  7. Ndipo Eliezeri mwana wa Dodavahu wa Maresha akatoa unabii dhidi ya Yehoshafati, akasema, “Kwa kuwa umeungana na Ahazia, Bwana ataangamiza vile mlivyotengeneza.” Zile meli zikavunjika na hazikuweza kungʼoa nanga ili kwenda Tarshishi.