Zaburi 81:6-16
6
Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao; mikono yao iliwekwa huru kutoka kwenye kikapu.
7
Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa, nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo; nilikujaribu katika maji ya Meriba.
8
“Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya: laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli!
9
Hamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu; msimsujudie mungu wa kigeni.
10
Mimi ni Bwana Mungu wako, niliyekutoa nchi ya Misri. Panua sana kinywa chako nami nitakijaza.
11
“Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza; Israeli hakutaka kunitii.
12
Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao wafuate mashauri yao wenyewe.
13
“Laiti kama watu wangu wangalinisikiliza, kama Israeli wangalifuata njia zangu,
14
ningaliwatiisha adui zao kwa haraka, na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao!
15
Wale wanaomchukia Bwana wangalinyenyekea mbele zake, na adhabu yao ingedumu milele.
16
Bali ninyi mngalilishwa ngano iliyo bora, na kuwatosheleza kwa asali itokayo kwenye mwamba.”
Settings