Skip to content
Zaburi 60:6-12

Zaburi 60:6-12

6
Mungu amenena kutoka patakatifu pake: “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi na kulipima Bonde la Sukothi.
7
Gileadi ni yangu na Manase ni yangu; Efraimu ni kofia yangu ya chuma, nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.
8
Moabu ni sinia langu la kunawia, juu ya Edomu natupa kiatu changu; nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”
9
Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?
10
Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu?
11
Tuletee msaada dhidi ya adui, kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.
12
Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, naye atawaponda adui zetu.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options