Zaburi 49:5-12
5
Kwa nini niogope siku mbaya zinapokuja, wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka,
6
wale wanaotegemea mali zao na kujivunia utajiri wao mwingi?
7
Hakuna mwanadamu awaye yote awezaye kuukomboa uhai wa mwingine, au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake.
8
Fidia ya uhai ni gharama kubwa, hakuna malipo yoyote yanayotosha,
9
ili kwamba aishi milele na asione uharibifu.
10
Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali zao.
11
Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, makao yao vizazi vyote; ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita kwa majina yao.
12
Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; anafanana na mnyama aangamiaye.
Settings