Skip to content
Zaburi 37:34-40

Zaburi 37:34-40

34
Mngojee Bwana, na uishike njia yake. Naye atakutukuza uirithi nchi, waovu watakapokatiliwa mbali, utaliona hilo.
35
Nimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi kama mwerezi wa Lebanoni,
36
lakini alitoweka mara na hakuonekana, ingawa nilimtafuta, hakupatikana.
37
Watafakari watu wasio na hatia, wachunguze watu wakamilifu, kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani.
38
Lakini watenda dhambi wote wataangamizwa, mafanikio yao yatakatiliwa mbali.
39
Wokovu wa wenye haki hutoka kwa Bwana, yeye ni ngome yao wakati wa shida.
40
Bwana huwasaidia na kuwaokoa, huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi, kwa maana wanamkimbilia.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options