Skip to content
Zaburi 37:21-33

Zaburi 37:21-33

21
Waovu hukopa na hawalipi, bali wenye haki hutoa kwa ukarimu.
22
Wale wanaobarikiwa na Bwana watairithi nchi, bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali.
23
Kama Bwana akipendezwa na njia ya mtu, yeye huimarisha hatua zake,
24
ajapojikwaa, hataanguka, kwa maana Bwana humtegemeza kwa mkono wake.
25
Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa au watoto wao wakiombaomba chakula.
26
Wakati wote ni wakarimu na hukopesha bila masharti. Watoto wao watabarikiwa.
27
Acha ubaya na utende wema, nawe utaishi katika nchi milele.
28
Kwa kuwa Bwana huwapenda wenye haki naye hatawaacha waaminifu wake. Watalindwa milele, lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali.
29
Wenye haki watairithi nchi, na kuishi humo milele.
30
Kinywa cha mwenye haki hutamka hekima, nao ulimi wake huzungumza lililo haki.
31
Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake; nyayo zake hazitelezi.
32
Watu waovu huvizia wenye haki, wakitafuta kuwaua;
33
lakini Bwana hatawaacha mikononi mwao wala hatawaacha wahukumiwe kuwa wakosa wanaposhtakiwa.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options