Skip to content
Zaburi 21:1-7

Zaburi 21:1-7

1
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako. Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake kwa ushindi unaompa!
2
Umempa haja ya moyo wake na hukumzuilia maombi ya midomo yake.
3
Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
4
Alikuomba maisha, nawe ukampa, wingi wa siku milele na milele.
5
Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa, umeweka juu yake fahari na utukufu.
6
Hakika umempa baraka za milele, umemfanya awe na furaha kwa shangwe ya uwepo wako.
7
Kwa kuwa mfalme anamtumaini Bwana; kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options