Nehemia 12:1-21
1
Hawa wafuatao walikuwa makuhani na Walawi ambao walirudi na Zerubabeli mwana wa Shealtieli pamoja na Yeshua: Seraya, Yeremia, Ezra,
2
Amaria, Maluki, Hatushi,
3
Shekania, Rehumu, Meremothi,
4
Ido, Ginethoni, Abiya,
5
Miyamini, Moadia, Bilga,
6
Shemaya, Yoyaribu, Yedaya,
7
Salu, Amoki, Hilkia na Yedaya. Hawa walikuwa viongozi wa makuhani na wenzao wakati wa Yeshua.
8
Walawi walikuwa Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na pia Matania, ambaye pamoja na wenzake, alikuwa kiongozi wa nyimbo za shukrani.
9
Bakbukia na Uni, wenzao, walisimama mkabala nao wakati wa ibada.
10
Yeshua alikuwa baba wa Yoyakimu, Yoyakimu alikuwa baba wa Eliashibu, Eliashibu alikuwa baba wa Yoyada,
11
Yoyada alikuwa baba wa Yonathani, na Yonathani alikuwa baba wa Yadua.
12
Katika siku za Yoyakimu, kulikuwa na wakuu wa jamaa za kikuhani: wa jamaa ya Seraya, Meraya; wa jamaa ya Yeremia, Hanania;
13
wa jamaa ya Ezra, Meshulamu; wa jamaa ya Amaria, Yehohanani;
14
wa jamaa ya Maluki, Yonathani; wa jamaa ya Shebania, Yosefu;
15
wa jamaa ya Harimu, Adna; wa jamaa ya Meremothi, Helkai;
16
wa jamaa ya Ido, Zekaria; wa jamaa ya Ginethoni, Meshulamu;
17
wa jamaa ya Abiya, Zikri; wa jamaa ya Miniamini na ya Maazia, Piltai;
18
wa jamaa ya Bilgai, Shamua; wa jamaa ya Shemaya, Yehonathani;
19
wa jamaa ya Yoyaribu, Matenai; wa jamaa ya Yedaya, Uzi;
20
wa jamaa ya Salu, Kalai; wa jamaa ya Amoki, Eberi;
21
wa jamaa ya Hilkia, Hashabia; wa jamaa ya Yedaya, Nethaneli.
Settings