Waamuzi 5:20-31
20
Kutoka mbinguni nyota zilipigana, nyota kutoka njia zake zilipigana na Sisera.
21
Mto wa Kishoni uliwasomba, ule mto wa zamani, mto wa Kishoni. Songa mbele, ee nafsi yangu, kwa ujasiri!
22
Ndipo kwato za farasi zikafanya mshindo: farasi wake wenye nguvu huenda mbio kwa kurukaruka.
23
Malaika wa Bwana akasema, ‘Merozi alaaniwe. Walaaniwe watu wake kwa uchungu, kwa kuwa hawakuja kumsaidia Bwana, kumsaidia Bwana dhidi ya hao wenye nguvu.’
24
“Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote, mkewe Heberi, Mkeni, abarikiwe kuliko wanawake wote waishio kwenye mahema.
25
Aliomba maji, naye akampa maziwa; kwenye bakuli la heshima akamletea maziwa mgando.
26
Akanyoosha mkono wake akashika kigingi cha hema, mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi. Akampiga Sisera kwa nyundo, akamponda kichwa chake, akamvunjavunja na kumtoboa paji lake la uso.
27
Aliinama miguuni pa Yaeli, akaanguka; akalala hapo. Pale alipoinama miguuni pake, alianguka; pale alipoinamia, ndipo alipoanguka, akiwa amekufa.
28
“Kupitia dirishani mamaye Sisera alichungulia; nyuma ya dirisha alilia, akasema, ‘Mbona gari lake linachelewa kufika? Mbona vishindo vya magari yake vimechelewa?’
29
Wanawake wenye busara kuliko wengine wote wakamjibu; naam, husema moyoni mwake,
30
‘Je, hawapati na kugawanya nyara: msichana mmoja au wawili kwa kila mtu, mavazi ya rangi mbalimbali kwa Sisera kuwa nyara, mavazi ya rangi mbalimbali yaliyotariziwa, mavazi yaliyotariziwa vizuri kwa ajili ya shingo yangu: yote haya yakiwa nyara?’
31
“Adui zako wote na waangamie, Ee Bwana! Bali wote wakupendao na wawe kama jua lichomozavyo kwa nguvu zake.” Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.
Settings