Yohana 9:30-41
30
Yule mtu akawajibu, “Hili ni jambo la ajabu! Hamjui anakotoka, naye amenifungua macho yangu!
31
Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii.
32
Tangu zamani hatujasikia kwamba mtu amemponya yeyote aliyezaliwa kipofu.
33
Kama huyu mtu hakutoka kwa Mungu, asingeweza kufanya lolote.”
34
Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa katika dhambi kabisa, nawe unajaribu kutufundisha?” Wakamfukuza atoke nje.
35
Yesu aliposikia kuwa wamemfukuzia nje yule mtu aliyemfumbua macho, alimkuta akamuuliza, “Je, unamwamini Mwana wa Adamu?”
36
Yule mtu akamjibu, “Yeye ni nani, Bwana? Niambie ili nipate kumwamini.”
37
Yesu akamjibu, “Umekwisha kumwona, naye anayezungumza nawe, ndiye.”
38
Yule mtu akasema, “Bwana, naamini.” Naye akamwabudu.
39
Yesu akasema, “Nimekuja ulimwenguni humu kwa ajili ya kuhukumu, ili wale walio vipofu wapate kuona, nao wale wanaoona, wawe vipofu.”
40
Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa karibu naye wakamsikia na kumwambia, “Je, kweli sisi ni vipofu?”
41
Yesu akawajibu, “Kama mngekuwa vipofu kweli, msingekuwa na hatia ya dhambi, lakini kwa kuwa mnasema, ‘Tunaona,’ basi mna hatia.
Settings