Skip to content
Ayubu 9:1-10

Ayubu 9:1-10

1
Kisha Ayubu akajibu:
2
“Naam, najua hili ni kweli. Lakini mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?
3
Ingawa mtu angetaka kushindana naye, asingaliweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja.
4
Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno. Ni nani aliyempinga naye akawa salama?
5
Aiondoa milima bila yenyewe kujua na kuipindua kwa hasira yake.
6
Aitikisa dunia kutoka mahali pake na kuzifanya nguzo zake zitetemeke.
7
Husema na jua, nalo likaacha kuangaza; naye huizima mianga ya nyota.
8
Yeye peke yake huzitandaza mbingu na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.
9
Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu, na Orioni, Kilimia, na makundi ya nyota za kusini.
10
Hutenda maajabu yasiyopimika, miujiza isiyoweza kuhesabiwa.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options