Ayubu 9:4-13
4
Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno. Ni nani aliyempinga naye akawa salama?
5
Aiondoa milima bila yenyewe kujua na kuipindua kwa hasira yake.
6
Aitikisa dunia kutoka mahali pake na kuzifanya nguzo zake zitetemeke.
7
Husema na jua, nalo likaacha kuangaza; naye huizima mianga ya nyota.
8
Yeye peke yake huzitandaza mbingu na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.
9
Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu, na Orioni, Kilimia, na makundi ya nyota za kusini.
10
Hutenda maajabu yasiyopimika, miujiza isiyoweza kuhesabiwa.
11
Anapopita karibu nami, siwezi kumwona; apitapo mbele yangu, simtambui.
12
Anapochukua kwa ghafula, ni nani awezaye kumzuia? Ni nani awezaye kumwambia, ‘Unafanya nini?’
13
Mungu hataizuia hasira yake; hata jeshi kubwa la Rahabu lenye nguvu linajikunyata miguuni pake.
Settings