Skip to content
Ayubu 41:9

Ayubu 41:9

Inaonyesha mstari 9 pamoja na muktadha unaouzunguka.
6
Je, wafanyabiashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake? Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara?
7
Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali, au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki?
8
Kama ukiweka mkono wako juu yake, utavikumbuka hivyo vita na kamwe hutarudia tena!
9
Tumaini lolote la kumtiisha ni kujidanganya; kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini.
10
Hakuna yeyote aliye mkali athubutuye kumchokoza. Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu?
11
Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa? Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu.
12
“Sitashindwa kunena juu ya maungo yake, nguvu zake na umbo lake zuri.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options