Ayubu 41:12-17
12
“Sitashindwa kunena juu ya maungo yake, nguvu zake na umbo lake zuri.
13
Ni nani awezaye kumvua gamba lake la nje? Ni nani awezaye kumsogelea na lijamu?
14
Nani athubutuye kuufungua mlango wa kinywa chake, kilichozungukwa na meno yake ya kutisha pande zote?
15
Mgongo wake una safu za ngao zilizoshikamanishwa imara pamoja;
16
kila moja iko karibu sana na mwenzake, wala hakuna hewa iwezayo kupita kati yake.
17
Zimeunganishwa imara kila moja na nyingine; zimengʼangʼaniana pamoja wala haziwezi kutenganishwa.
Settings