Skip to content
Ayubu 41:13-25

Ayubu 41:13-25

13
Ni nani awezaye kumvua gamba lake la nje? Ni nani awezaye kumsogelea na lijamu?
14
Nani athubutuye kuufungua mlango wa kinywa chake, kilichozungukwa na meno yake ya kutisha pande zote?
15
Mgongo wake una safu za ngao zilizoshikamanishwa imara pamoja;
16
kila moja iko karibu sana na mwenzake, wala hakuna hewa iwezayo kupita kati yake.
17
Zimeunganishwa imara kila moja na nyingine; zimengʼangʼaniana pamoja wala haziwezi kutenganishwa.
18
Akipiga chafya mwanga humetameta; macho yake ni kama mionzi ya mapambazuko.
19
Mienge iwakayo humiminika kutoka kinywani mwake; cheche za moto huruka nje.
20
Moshi hufuka kutoka puani mwake, kama kutoka kwenye chungu kinachotokota kwa moto wa matete.
21
Pumzi yake huwasha makaa ya mawe, nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake.
22
Nguvu hukaa katika shingo yake; utisho hutangulia mbele yake.
23
Mikunjo ya nyama yake imeshikamana imara pamoja; iko imara na haiwezi kuondolewa.
24
Kifua chake ni kigumu kama mwamba, kigumu kama jiwe la chini la kusagia.
25
Ainukapo, mashujaa wanaogopa; hurudi nyuma mbele yake anapokwenda kwa kishindo.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options