Ayubu 41:1-9
1
“Je, waweza kumvua Lewiathani kwa ndoano ya samaki, au kufunga ulimi wake kwa kamba?
2
Waweza kupitisha kamba puani mwake, au kutoboa taya lake kwa kulabu?
3
Je, ataendelea kukuomba umhurumie? Atasema nawe maneno ya upole?
4
Je, atafanya agano nawe ili umtwae awe mtumishi wako maisha yake yote?
5
Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege, au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako?
6
Je, wafanyabiashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake? Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara?
7
Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali, au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki?
8
Kama ukiweka mkono wako juu yake, utavikumbuka hivyo vita na kamwe hutarudia tena!
9
Tumaini lolote la kumtiisha ni kujidanganya; kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini.
Settings