Skip to content
Ayubu 40:20-28

Ayubu 40:20-28

20
Vilima humletea yeye mazao yake, nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye.
21
Hulala chini ya mimea ya yungiyungi, katika maficho ya matete kwenye matope.
22
Hiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake; miti mirefu karibu na kijito humzunguka.
23
Wakati mto ufurikapo, yeye hapati mshtuko wa hofu; yeye yu salama, hata kama Yordani ingefurika hadi kwenye kinywa chake.
24
Je, mtu yeyote anaweza kumkamata yeye akiwa macho, au kumnasa kwa mtego na kutoboa pua yake?
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options