Skip to content
Ayubu 40:1-9

Ayubu 40:1-9

1
Bwana akamwambia Ayubu:
2
“Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha? Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.”
3
Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:
4
“Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe? Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu.
5
Nimesema mara moja, lakini sina jibu; naam, nimesema mara mbili, lakini sitasema tena.”
6
Ndipo Bwana akasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli:
7
“Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu.
8
“Je, utabatilisha hukumu yangu? Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe?
9
Je, una mkono kama wa Mungu, nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake?
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options