Ayubu 40:1-5
1
Bwana akamwambia Ayubu:
2
“Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha? Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.”
3
Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:
4
“Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe? Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu.
5
Nimesema mara moja, lakini sina jibu; naam, nimesema mara mbili, lakini sitasema tena.”
Settings