Ayubu 35:9-16
9
“Wanadamu hulia kwa kulemewa na mateso; huomba msaada kutoka mkono wenye nguvu.
10
Lakini hakuna asemaye, ‘Yuko wapi Mungu Muumba wangu, yeye anifanyaye niimbe usiku,
11
yeye atufundishaye sisi zaidi kuliko wanyama wa dunia, na kutufanya wenye hekima kuliko ndege wa angani?’
12
Yeye hajibu wakati watu waliapo kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.
13
Naam, Mungu hasikilizi maombi yao ya ubatili; Mwenyezi hayazingatii.
14
Si zaidi sana kwamba hatakusikiliza wewe usemapo humwoni, tena ya kwamba shauri lako liko mbele zake na wewe lazima umngojee,
15
pia zaidi, kwamba hasira yake kamwe haiadhibu wala haangalii uovu hata kidogo?
16
Hivyo Ayubu hufumbua kinywa chake kwa maneno yasiyo na maana; anaongea maneno mengi bila maarifa.”
Settings