Ayubu 30:1-8
1
“Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuniliko wananidhihaki, watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo.
2
Nguvu za mikono yao zingekuwa na faida gani kwangu, kwa kuwa nguvu zao zilikuwa zimewaishia?
3
Wakiwa wamekonda kutokana na kupungukiwa na kwa njaa, walizurura usiku katika nchi kame iliyo ukiwa.
4
Katika vichaka walikusanya mimea ya chumvi, nacho chakula chao kilikuwa mizizi ya mti wa mfagio.
5
Walifukuzwa mbali na watu wao, wakipigiwa kelele kama wevi.
6
Walilazimika kuishi katika mikondo ya vijito vilivyokauka, kwenye majabali na mahandaki.
7
Kwenye vichaka walilia kama punda, na walijisongasonga pamoja kwenye vichaka.
8
Wao ni watoto wa wapumbavu wenye asili ya ubaya, waliofukuzwa watoke katika nchi.
Settings