Ayubu 22:21-30
21
“Mjue sana Mungu ili uwe na amani, ndipo mema yatakapokujia.
22
Uyapokee mafundisho toka kinywani mwake, na maneno yake uyaweke moyoni mwako.
23
Kama ukimrudia Mwenyezi, utarudishwa upya: Kama ukiuondoa uovu uwe mbali na hema lako,
24
kama dhahabu yako ukiihesabu kama mavumbi, dhahabu yako ya Ofiri kama miamba ya mabondeni,
25
ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako, naye atakuwa fedha yako iliyo bora.
26
Hakika ndipo utakapojifurahisha kwa Mwenyezi, nawe utamwinulia Mungu uso wako.
27
Utamwomba yeye, naye atakusikia, nawe utazitimiza nadhiri zako.
28
Utakusudia jambo nalo litatendeka, nao mwanga utaangazia njia zako.
29
Watu watakaposhushwa, nawe ukasema, ‘Wainue!’ ndipo atamwokoa aliyevunjika moyo.
30
Atamwokoa hata yule ambaye ana hatia, ataokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako.”
Settings