Ayubu 15:7-16
7
“Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa? Ulizaliwa kabla ya vilima?
8
Je, wewe husikiliza mashauri ya siri ya Mungu? Je, wewe unaizuia hekima iwe yako mwenyewe?
9
Wewe unajua kitu gani tusichokijua sisi? Unafahamu kitu gani tusichokifahamu sisi?
10
Wale wenye mvi na wazee wako upande wetu, watu ambao ni wazee hata kuliko baba yako.
11
Je, faraja za Mungu hazikutoshi, au maneno yaliyosemwa kwako kwa upole si kitu?
12
Kwa nini moyo wako unakudanganya, na kwa nini macho yako yanangʼaa,
13
ili kwamba upate kutoa hasira yako dhidi ya Mungu, na kumwaga maneno kama hayo kutoka kinywani mwako?
14
“Mwanadamu ni kitu gani, hata aweze kuwa safi, au yeye aliyezaliwa na mwanamke, hata aweze kuwa mwadilifu?
15
Kama Mungu hawaamini watakatifu wake, kama hata mbingu zenyewe si safi machoni pake,
16
sembuse mwanadamu ambaye ni mwovu na mpotovu, ambaye hunywa uovu kama anywavyo maji!
Settings