Ayubu 10:2-13
2
Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu.
3
Je, inakupendeza wewe kunionea, kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu?
4
Je, wewe una macho ya kimwili? Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo?
5
Je, siku zako ni kama zile za mwanadamu, au miaka yako ni kama ile ya mtu,
6
ili kwamba utafute makosa yangu na kuichunguza dhambi yangu;
7
ingawa wajua kuwa mimi sina hatia, na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako?
8
“Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya. Je, sasa utageuka na kuniangamiza?
9
Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi. Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena?
10
Je, wewe hukunimimina mimi kama maziwa, na kunigandisha kama jibini,
11
ukanivika ngozi na nyama, na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa?
12
Umenipa uhai na kunitendea wema, katika uangalizi wako umeilinda roho yangu.
13
“Lakini hili ndilo ulilolificha moyoni mwako, nami ninajua kuwa hili lilikuwa katika nia yako:
Settings