Ayubu 10:1-7
1
“Nayachukia sana haya maisha yangu; kwa hiyo nitatoa malalamiko yangu kwa wazi bila kujizuia, nami nitanena kutokana na uchungu wa moyo wangu.
2
Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu.
3
Je, inakupendeza wewe kunionea, kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu?
4
Je, wewe una macho ya kimwili? Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo?
5
Je, siku zako ni kama zile za mwanadamu, au miaka yako ni kama ile ya mtu,
6
ili kwamba utafute makosa yangu na kuichunguza dhambi yangu;
7
ingawa wajua kuwa mimi sina hatia, na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako?
Settings